Skip to content

Alive Quote by Enock Maregesi

“Mungu alikuumba miaka mingi kabla hujazaliwa. Ndani ya roho yako kulikuwa na mpango mkuu wa Mungu juu ya maisha yako katika kipindi chote utakachokuwa hai, na katika kipindi chote utakachokuwa mfu. Lakini Shetani katika mji wa angani unaosemekana kuzuia majibu ya maombi ya Danieli ya siku ishirini…” quote by Enock Maregesi
Download Open image
““Mungu alikuumba miaka mingi kabla hujazaliwa. Ndani ya roho yako kulikuwa na mpango mkuu wa Mungu juu ya maisha yako katika kipindi chote utakachokuwa hai, na katika kipindi chote utakachokuwa mfu. Lakini Shetani katika mji wa angani unaosemekana kuzuia majibu ya maombi ya Danieli ya siku ishirini na moja, kutoka mbinguni kuja duniani, uitwao Sadiki, wenye mashetani wenye nguvu kuliko mashetani wote katika ufalme wa giza, akaizuia roho hiyo kisha akaiwekea mpango mkuu wa Shetani juu ya maisha yako ili umtumikie yeye badala ya kumtumikia Mwenyezi Mungu. Kwa mfano, Mungu alipanga uzaliwe mkoani Arusha. Halafu akapanga mke au mume wako azaliwe mkoani Mwanza. Mkoani Arusha Mungu alipanga uwe mwinjilisti wa vitabu, wakati mkoani Mwanza alipanga mke au mume wako awe mwimbaji wa nyimbo za injili. Katika mikoa yote miwili Mungu alishatuma malaika wema wa kuwasaidia katika mipango mikuu ya maisha yenu na kuwaepusha na hila zote za adui. Lakini badala ya kuzaliwa Arusha au Mwanza Shetani ataziprogramu roho zenu upya ili wa Arusha azaliwe Dodoma au Mara au Venezuela na wa Mwanza azaliwe Lindi au Kagera au Mombasa, ambapo hakutakuwa na malaika wema wa kuwasaidia. Badala ya kuwa mwinjilisti wa vitabu, Shetani atakufanya uwe jambazi; na badala ya kuwa mwimbaji wa nyimbo za injili, Shetani atakufanya uwe mwanamuziki. Ndiyo maana wakati mwingine ni vizuri kuhama sehemu unapoishi na kwenda kuishi sehemu nyingine, ambapo kwa kusaidiana na malaika wako wa mwanzo ambaye Mungu alikupangia kabla hujazaliwa, utafanikiwa katika maisha yako, kama alivyofanya Ibrahimu. Watu wengi wanaishi maisha ambayo si ya kwao. Kukomboa kile ambacho Mungu alikipanga ndani ya roho yako kabla hujazaliwa, na kabla roho yako haijazuiwa na mashetani wa angani, kuwa karibu na Mwenyezi Mungu. Kwa Mungu hakuna siri, atakufunulia tu.””

Enock Maregesi

About This Quote

Life’s path is shaped by divine plans, yet demonic influences may divert destiny; aligning with higher purpose brings success.

In simple terms: Follow divine guidance, resist negative forces.

Key Takeaway

Stay true to your purpose.

Themes

faith destiny spiritual warfare

Mood

determined spiritual

Type

philosophical motivational

When to use this quote

  • career choices
  • marriage
  • spiritual practice
  • community building

Key Concepts

divine plan temptation free will

Questions to Reflect On

  • What steps align you with your intended path?
  • How do you recognize and resist negative influences?
A Different Perspective

Human agency can reshape outcomes.

3.3 out of 5 (5 ratings)

More by Enock Maregesi

Explore all 471 Enock Maregesi quotes

More Alive quotes

Browse all 7,282 Alive quotes