Chuo Quote by Enock Maregesi
““Kamishna … karibu," alisema Nafi huku akisimama na kutupa gazeti mezani na kuchukua karatasi ya faksi, iliyotumwa. "Ahsante. Kuna nini …" "Kamishna, imekuja faksi kutoka Oslo kama nilivyokueleza – katika simu. Inakutaka haraka, kesho, lazima kesho, kuwahi kikao Alhamisi mjini Copenhagen," alisema Nafi huku akimpa kamishna karatasi ya faksi. "Mjini Copenhagen!" alisema kamishna kwa kutoamini. "Ndiyo, kamishna … Sidhani kama kuna jambo la hatari lakini." "Nafi, nini kimetokea!" "Kamishna … sijui. Kwa kweli sijui. Ilipofika, hii faksi, kitu cha kwanza niliongea na watu wa WIS kupata uthibitisho wao. Nao hawajui. Huenda ni mauaji ya jana ya Meksiko. Hii ni siri kubwa ya tume kamishna, na ndiyo maana Oslo wakaingilia kati." "Ndiyo. Kila mtu ameyasikia mauaji ya Meksiko. Ni mabaya. Kinachonishangaza ni kwamba, jana niliongea na makamu … kuhusu mabadiliko ya katiba ya WODEA. Hakunambia chochote kuhusu mkutano wa kesho!" "Kamishna, nakusihi kuwa makini. Dalili zinaonyesha hali si nzuri hata kidogo. Hawa ni wadhalimu tu … wa madawa ya kulevya." "Vyema!" alijibu kamishna kwa jeuri na hasira. Halafu akaendelea, "Kuna cha ziada?" "Ijumaa, kama tulivyoongea wiki iliyopita, nasafiri kwenda Afrika Kusini." "Kikao kinafanyika Alhamisi, Nafi, huwezi kusafiri Ijumaa …" "Binti yangu atafukuzwa shule, kam …" "Nafi, ongea na chuo … wambie umepata dharura utaondoka Jumatatu; utawaona Jumanne … Fuata maadili ya kazi tafadhali. Safari yako si muhimu hivyo kulinganisha na tume!" "Sawa! Profesa. Niwie radhi, nimekuelewa, samahani sana. Samahani sana.””
About This Quote
A tense conversation reveals a secret fax about a possible murder in Mexico, political intrigue, and a planned meeting in Copenhagen, highlighting danger and mistrust.
In simple terms: A secret fax hints at murder and political danger.
Beware hidden threats.
Themes
Mood
Type
When to use this quote
- international diplomacy
- law enforcement
- journalistic investigation
Key Concepts
Questions to Reflect On
- What risks are involved in sharing this fax?
- How might the meeting in Copenhagen affect the situation?
The truth may be concealed and dangerous.