Bob Riza Quotes
- Njaa haina rangi kiasi kwamba utaiona kwa macho
- Hasira zinaweza kumfanya mtu achukue uamuzi wowote ule 'mbaya au mzuri''
- Maisha yangekuwa sumu watu wengi tungekufa
- Mawazo hayapimwi kwa mzani
- Mke hanapenda mabusu na sio makofi
- Ujinga wa wachawi ni kwamba hawakuibii mali wala pesa bali kukukaba na kukutesa tu
- Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu
- Hata raisi naye huwa anaenda msalani na anafurahi au kununa kama mtu wa kawaida
- Wanasema ukikalia mafiga ni vibaya kwa mtoto wa kiume ''mababu hao
- Tatizo lisikie kwa mwenzako tu...likikupata wewe utakiona cha moto
- Mpiganaji hupata kidogo kitu sio sawa na mkaa bure
- Mimi nina sumu kama kifutu hivyo usije na kisu butu
- Kamwe panga haliwezi kukaa kwenye pochi
- Rafiki ni yule akufaaye kwenye dhiki
- Hakuna binadamu mwenye mamlaka sawa na mungu
- Kamwe chupi haivaliwi miguuni
- Hakuna makalio yaliyochongoka 'nenda popote pale duniani hutoyakuta
- Mchawi wako anaweza kuwa hata ndugu yako wa damu
- Mama ni mama hata akiwa kilema
- Raha ya mapenzi ni kuwa huru na sio uwoga na wasiwasi