“Lakini, akiendelea kuwaza na kuangaza, ghafla Murphy aliona kitu kama gari likiwa limesimama kwa mbali. Alisimama na kupata hamu ya kujua. Murphy alianza tena kutembea, lakini sasa akiifuata ile gari, halafu akaongeza mwendo na kukimbia; macho yote yakiwa mbele! Alipofika, karibu na gari ile, hakuminya kifyatulio kumpiga mtu risasi. Alijenga tabasamu na kuongeza mwendo. Gari ilikuwa Ferrari Testarrosa ya Lisa… — Enock Maregesi Copy Share
“Kilometa mbili na ushei kidogo kutoka katika sanamu la Yesu Mtoto liitwalo Niñopa, katika Kanisa la Parokia ya Manispaa ya Xochimilco ('Sochimiliko') la Iglesia de San Bernardino de Siena, Mexico City, kulikuwa na nyumba ndogo ya siri ('safe house') ya Kolonia Santita iliyojengwa bila uzio wa ukuta au seng’enge isipokuwa miti iliyopandwa kuizunguka bila mpangilio wowote. Ndani ya nyumba hiyo… — Enock Maregesi Copy Share
“Polisi wa kituo cha kati cha Coyoacán kumbe hawakuwa mbali na sehemu zile. Walipoona gari zikifukuzana waliona ujanja ni kuwakatisha Vijana wa Tume katika vichochoro. Haikuchukua muda magari sita ya polisi yalitokeza Vallarta (Barabara ya Vallarta) na kuliona gari la Vijana wa Tume Gómez Farías likipepea kwa mwendo mkali kuelekea Cuauhtémoc, na gari za magaidi kwa nyuma yao. Kwa vile… — Enock Maregesi Copy Share
“Murphy. Sina mbinu zozote za kujikinga kama unavyojua; mbali na mafunzo ya FBI. Baada ya kumrusha nyoka wa Lisa nywele zilinisisimka. Wazo… — Enock Maregesi Copy Share Image